Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Seneta Nasser Abbas Jafari, Raisi wa Baraza la Umoja wa Waislamu Pakistani, akiwa pamoja na ujumbe wa wajumbe wa baraza hilo katika safari rasmi ya Najaf Ashraf, amekutana na Ayatullah al-Udhma Hafidh Bashir Hussein Najafi na kufanya mazungumzo ya pamoja.
Katika kikao hicho, Ayatullah al-Udhma Bashir Najafi, pamoja na kuukaribisha ujumbe wa Kipakistani, akabainisha nafasi mashuhuri ya Hawza ya Najaf Ashraf, akataja ukubwa wake wa kielimu, nafasi yake ya kihistoria na huduma kubwa za wanazuoni waliokuzwa katika Hawza hii, pia alisisitiza juu ya majukumu mazito ya wanazuoni wa leo na umuhimu wa kuongoza Umma wa Kiislamu kwa usahihi katika mazingira nyeti ya sasa.
Aidha, Seneta Nasser Abbas Jafari, kwa kuithamini fursa ya kukutana na Marja’ mkubwa, alisema uwepo wa Ayatullah Bashir Najafi ni neema kubwa kwa Umma wa Kiislamu na hususan Waislamu wa Bara Dogo la India, Aliongeza kuwa uwepo wa Marja’iyyah ni chanzo cha matumaini kwetu, na ofisi ya Mtukufu huyo inafanya kazi kama kivuli cha uhakika kwa Umma wa Kiislamu na eneo la Bara Dogo, heshima na hadhi yetu inategemea uwepo na miongozo yake.
Mwishoni mwa kikao hiki, Raisi wa Baraza la Umoja wa Waislamu Pakistani alimshukuru Ayatullah al-Udhma Bashir Najafi kwa kutenga muda wake wenye thamani kwa ajili ya kikao hiki cha kirafiki.
Maoni yako